Thursday, August 23, 2012

KUSHOTO TAZNEEM,KATIKATI OMMY DIMPOZ NA KULIA PAH ONE

 Utajiuliza kwanini nimewaweka katika pande tofauti,lakini ukweli ni kuwa ni wasanii ambao ni wapya kabisa (Up coming Artists) katika fani ya muziki wa Bongo Fleva .
Tazneem mimi ninamwona kama msanii mwenye tofauti kubwa na wasanii wengine. Kwanza pamoja na kuwa ni mtanzania ambaye ana asili ya kiasia, pia ni msanii wa kike ambaye amekuja na style ya muziki iliyo ya kipekee. Na anaonesha kuwa anao uwezo wa kuwa inspire wasanii wengine wa kike.
Ukitazama Video ya wimbo wake wa 'Kwasakwasa' utaweza kugundua uwezo ambao ameuonesha. Ingawa pia kwa kiwango kikubwa Producer wa wimbo amefanya kazi yake,lakini pia Tazneem ameonesha uwezo wake. Na hata kampuni iliyotengeneza video ya I-View nayo imefanya kazi yake nzuri. 'Congratulation to Audio Producers,Singer na Video Director'.

Nikija upande wa Ommy Dimpoz,kwa upande wangu nadhani alipotoka na wimbo wake wa 'nai nai' wengi wetu hatukumwamini sana. Hata mimi sikuamini kama anaweza akatoa track nyingine ambayo ingeweza kuwa kali. Na kwa upande wangu ninaiona track ya pili ya 'baadae' kama ni kali zaidi ya ile ya kwanza au zipo katika kiwango kimoja, kitu ambacho wasanii wengi uwa wanashindwa. Na nimeipenda hata idea yake ya kufanyia video ya wimbo wake wa 'baadae' huko South Africa na akimtumia Director wa hapa hapa bongo Adam Juma. Hakuna ubishi kuwa kwa sasa Adam Juma ni director wa video za muziki ambaye yupo kwenye level za tofauti na directors wengine wa bongo na ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Namalizia na Pah One ni kundi la muziki wa bongo fleva ambalo linaonekana kuwa na syle tofauti na makundi mengine ya muziki ya hapa bongo. Ukitazama namna wanavyovaa, tattoo na hata style zao za nywele. Ila nataka tusubirie track zao zitakazofuata ndio tutaweza kuwahukumu vyema zaidi. Nilichokipenda ni video ya wimbo wao wa 'ghetto'ambayo wamefanya kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Ila tu katika upande wa audio jamaa wanaonekana kuiga syle za wasanii wa afrika kusini. Kwa ukweli sijaona jipya sana.



No comments:

Post a Comment