Thursday, November 3, 2011

ALI KIBA UPO WAPI?


Jamaa alianza kitambo sana,tangu enzi hizo Mr Blue na Ab Skills ana shine na wakafanya wimbo wa 'Maria' Baadae jamaa akaja akatoka ki ukweli na nyimbo kali kama Cinderela,MackMuga na nyingine kali. Akafanya wimbo na Wasanii kadhaa akiwemo R-Kelly ulioitwa 'Hands across the world'. Ila mimi nilitegemea angetumia nafasi hiyo kwenda kwenye level ambayo ni ya kimataifa zaidi,ila wapi? Ali Kiba sasa hivi ana wimbo wake unaoitwa  'Dushelele' wimbo ni mzuri ila video yake kwa upande wangu sijaikubali kabisa.
UNAFAHAMU SABABU ZA MIMI KUTOIKUBALI VIDEO YA WIMBO ULE?
Sababu mojawapo ni rangi,kwa kweli rangi katika ile video sio nzuri katika kiwango kinachotakiwa. Hata kwa upande wa ubora,inaonekana haina ubora wa kuridhisha. Maoni yangu kwa Ali Kiba,ni kuwa anapaswa kujiboresha zaidi katika upande wa kufanya audio na video kali. Lakini pia 'promotion'inahitajika zaidi kuelekea katika level za kimataifa kwani nafasi anayo,tena kubwa zaidi.
TAZAMA VIDEO YA DUSHELELE YA ALI KIBA

No comments:

Post a Comment