Thursday, August 23, 2012


JE UNAYAFAHAMU MADHARA YA KUTUMIA DEODORANTS?


Mara nyingi wengi wetu kila baada ya kuoga na tunapokuwa na mtoko,iwe asubuhi au jioni tunapendelea kutumia deodorant katika makwapa na hata nguo kwa lengo la kuzuia harufu mbaya ya jasho. Na tumekuwa tukifanya hivyo kwa kipindi kirefu sana.
JE UNAFAHAMU MADHARA YAKE?
HAYA NDIO MADHARA YAKE:

MADOA KWENYE NGUO: Inachukua kiasi cha sekunde 30 kwa yale majimaji ya deodorant uliyopakaa kuyeyuka katika ngozi ya mwili wako. Hivyo basi kama utapakaa deodorant katika ngozi ya mwili wako na ukavaa nguo kabla hata yale majimaji hayajakauka,inaweza kusababisha yale majimaji yakagusana na nguo na hatimaye yakatengeneza madoa sugu kwenye nguo yako. Na mara nyingi Deodorant zenye ute mweupe ndio ambazo ni hatari kwa nguo kutokana na madoa yake kuwa sugu.

MADHARA YA KIAFYA: Deodorants nyingi zina 'Aluminum zirconium' ambazo zinasemekana kuwa na uwezekano wa kusababisha matatizo ya kiafya kama Anaemia,magonjwa ya mifupa na kuchanganyikiwa.

MADHARA KWENYE NGOZI: Jasho kwenye mwili halina harufu ila wale bakteria ambao wanatumia jasho kama chakula ndio wanaharufu mbaya. Hivyo basi Deodorant inasaidia kufanya mwili wako kuwa acid na kupambana na bakteria. Hivyo basi Deodorant zinaweza kusababisha ngozi ya mwli wako kuwa kavu sana.

Inashauriwa kutumia Deodorant ambazo hazina viambata vya alcoholic(alcoholic free spray) ambazo baadhi ya wataalamu wanasema huwa hazina aliminium na pia zinakuwa hazina allerges au irritations.
Pia inaelezwa kuwa deodorant zenye maji maji ni bora zaidi ya zile za kupuliza(spray) kwa sababu spray zina kuwa zina kemikali zenye kutoa marashi kwa muda mrefu tofauti na hizi zenye majimaji.
 Epuka Deodorant za bei nafuu kwa sababu itakusaidia kutotumia pesa nyingi ila inaweza kukusababishia madhara kwenye ngozi yako na afya yako kwa ujumla.




No comments:

Post a Comment