Wednesday, October 26, 2011

JE UNATAMBUA KUWA SIMU YAKO YA MKONONI NI CHAFU SANA KULIKO HATA CHOO?


Mara nyingi sana watu wengi tuna tabia ya kusafisha mikono yetu baada ya kutoka chooni. Tunasahau kuwa wakati mwingine tunaingia huko chooni na simu zetu za mkononi,na hata kusoma sms au kutuma sms tukiwa chooni. Na tunapotoka chooni tunasafisha mikono yetu na kujiona kuwa tumeshakuwa katika hali ya usafi huku tukisahau kuwa tuliingia na simu zetu za mkononi huko chooni tulipokuwa.
Utafiti  mmoja umefanywa huko Uingereza,ambapo wataalamu walichukua watu 390 pamoja na simu zao za mkononi. Na hatimaye waligundua kuwa asilimia 92 ya watu waliokuwa na simu hizo waligundulika kuwa na Bakteria na asilimia 82 ya simu ziligundulika kuwa na Bakteria. Na mojawapo ya bakteria hao ni 'staphylococcus aureus' ambao wana madhara kwenye baadhi ya sehemu za mwili kama macho na kwenye ngozi.
Na je unawezaje kujikinga na Bakteria hao? Imeshauriwa kusafisha mikono kila baada ya kutoka chooni.  Na pia inashauriwa watu kuwa na tabia ya kusafisha simu zao angalau mara moja kwa wiki kwa kutumia kipande cha pamba kilichochovywa kwenye ''Rubbing Alcohol''

No comments:

Post a Comment