Monday, October 24, 2011

UNAMKUMBUKA MC HAMMER? SASA YUPO KWENYE LIGI NA WAMILIKI WA GOOGLE


Mc Hammer sasa ameingia kwenye mambo ya teknolojia baada ya kutangaza kuanzisha search engine iitwayo 'WireDoo'. Mc Hammer alitangaza kuanzishwa kwa search engine hiyo katika mkutano mkubwa unaoitwa WEB 2.0 huko San Fransisco Marekani. Kwa mujibu wa Mc Hammer amesema WireDoo itakuwa inatumika kutafuta topiki au vitu mbalimbali mfano magari na vitu vingine tofauti.
Mc Hammer ambaye alikuwa ni mkali wa Hiphop aliyefunika mbaya miaka hiyo? kwa sasa anajishughulisha na mambo ya teknolojia. Na ameshaudhuri  kwenye vyuo mbalimbali kutoa mihadhara (presentations) ikiwemo Oxford University cha England na Harvard cha Marekani.
Kwa sasa hivi Google ndio kila kitu,pale unapozungumzia social engine kali. Je WireDoo inaweza ikaipiga bao Google????

No comments:

Post a Comment