Wednesday, October 26, 2011

NDEGE YA KIPEKEE;BOEING 787 DREAMLINER SASA IMEANZA SAFARI


BOEING 787 DREAMLINER ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na wadau wa Teknolojia duniani sasa imezinduliwa rasmi mjini Tokyo nchini Japani. Na imeanza safari zake kwa huko huko Japan katika miji ya Okayama na Hiroshima. Ndege hiyo iliyotengenezwa kipekee na material ya carbon fiber-reinforced plastic ikiwa inatumia mafuta kidogo kulinganisha na ndege nyingine za Boeing kwa takribani pungufu ya 20%. Hata madirisha yake ni makubwa kuliko ya Boeing 767 na yanapitisha mwanga wa kutosha na nindege yenye kuingiza hewa ya kutosha kulinganisha na ndege nyingine. Na pia ina uwezo wa kusafiri kilomita 15000 bila kutua mahali popote. Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege liitwalo ANA ambalo limeagiza ndege nyingine kama hizo 55.

No comments:

Post a Comment