Saturday, July 9, 2011

ALMUNIA NA BENDTNER UENDA WAKAONDOKA ARSENAL?


Wakali wa Arsenal golikipa Manuel Almunia,34 na mshambuliaji Nicklas Bendtner,23 wako katika mazungumzo na klabu mbili tofauti za  mpira. Ingawa haijawekwa wazi ni klabu gani hizo ambayo ina nia ya kuwasajili lakini msemaji wa klabu ya Arsenal amedhibitisha hayo na kusema bado wapo kwenye majadiliano na klabu hiyo na iwapo dau litafikiwa basi Arsenal itakubali kuwauza. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anatarajia kulizungumzia suala hilo wiki ijayo pale atakapokutana na waandishi wa habari.
Wachezaji hao wameachwa katika ziara ya timu hiyo katika bara la Asia. Wengine walioachwa ni pamoja na Naodha wa timu hiyo Cesc Fabregas ambaye ni mgonjwa, mlinzi Emmanuel Eboue. Kiungo Samir Nasri imeripotiwa kuwa yupo katika msafara huo licha ya tetesi za kutaka kusajiliwa na klabu nyingine kali kama Manchester United na Chelsea. Kama Almunia na Bendtner wataondoka Arsenal watakuwa ni miongoni mwa nyota watatu waliouzwa na klabu hiyo kufuatia Gael Clichy ambaye amesajiliwa na klabu ya Manchester city kwa ada ya paundi milioni sita.

No comments:

Post a Comment