Saturday, July 9, 2011

GUNNERS WAENDELEA KUWANGANGANIA FABREGAS NA NASRI


Klabu ya soka ya Arsenal imeendelea kuwangangania wachezaji wake Cesc Fabregas na Samir Nasri,huku Meneja wa timu hiyo Arsene Wenger akishikilia msimamo wake kuwa hayuko tayari kuwaachia wachezaji hao hata kwa dau lolote lile. Cesc Fabregas amekuwa akitakiwa na Barcelona huku Samir Nasri akitakiwa na Manchester United. Na hivi karibuni Manchester United walisema wako tayari kumnunua Nasri kwa dau la Paundi milioni 20 lakini Arsenal imeendelea kukataa kumuachia mchezaji huyo. Wakati huohuo Nasri amekataa kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambapo amebakisha miezi 12 tu kuendelea kuichezea klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment