Monday, September 12, 2011

NOKIA 1100 a.k.a NOKIA YA TOCHI; ''UNAIKUMBUKA??''

Nokia 1100 maarufu kama Nokia ya tochi ndio simu iliyouza kuliko simu zote zilizowahi kuzalishwa humu ulimwenguni. Simu hii ilitengenezwa mwaka 2003 na ilibuniwa na mmarekani mwenye asili ya Bulgaria anayeitwa
Miki Mehandjiysky. Kwa sasa Nokia hawaendelei kuzalisha tena modeli ya simu hii. Mpaka sasa hakuna aina nyingine ya simu iliyouza kuliko hii Nokia 1100 a.k.a Nokia ya tochi. Mpaka inaachwa kutengenezwa mwaka 2009 jumla ya simu milioni 250 zilikuwa zimeuzwa. UNAAMINI?? Hakuna aina nyingine ya simu iliyowahi kuzalishwa na Nokia au kampuni nyingine yoyote ikafikia kiwango hicho cha mauzo.

No comments:

Post a Comment