Tuesday, October 18, 2011

BLACKBERRY INAZIDI KUPOTEZA MVUTO AU TATIZO NINI?


Mmoja kati ya watumiaji watano wa BlackBerry ambaye alipata matatizo ya mawasiliano wiki nzima iliyopita amedai kuna akaacha kutumia aina hiyo ya simu. Hii ni baada ya mamilioni ya watumiaji wa BlackBerry kukosa mawasiliano ya internet kwa takribani wiki nzima iliyopita. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa kwa zaidi ya watu 1000 na mtandao wa kelkoo imeonekana kuwa 8% tayari wameshaacha kutumia BlackBerry,huku 19% wakidai wanafikiria kuachana na matumizi ya BlackBerry na 42% wakidai uenda wakaachana na BlackBerry hapo baadae iwapo itaendelea kuwa na matatizo . Katika nchi za ulaya na Marekani baada ya uzinduzi wa Iphone 4S ambayo ni aina mpya ya simu kutoka Apple tayari idadi ya wanaohitaji aina hiyo ya simu imeongezeka sana na kufikia milioni moja hususani baada ya watumiaji wa BlackBerry kukumbwa na matatizo ya mawasiliano wiki iliyopita. Hivi karibuni kampuni ya RIM ambayo inatengeneza BlackBerry imeomba radhi kwa watumiaji wake na kuahidi kutoa software mpya bure kwa watumiaji wake kama ishara ya kuonyesha kuwajali. Lakini kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya mawasiliano wamedai hilo haliwezi kuwasaidia BlackBerry katika kukuza mauzo yake,kwani  watumiaji wengi wa BlackBerry ni wafanyabiashara ambao mawasiliano kwa njia ya internet ni muhimu kwao.
Hata hivi karibuni thamani ya hisa za BlackBerry inaonekana kushuka kwa kasi.

No comments:

Post a Comment