Kesho siku ya Jumatano ( August 31) rapa kutoka USA T.I atakuwa anaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miezi 11 katika gereza la Forrest City, Arkansas huko huko Marekani. T.I alihukumiwa kifungo cha miezi 11 baada ya kukutwa na madawa ya kulevya kwenye gari mnamo Septemba 2010, ikiwa ni miezi 6 tu baada ya kutoka jela alipokuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja. Tunasubiri kuona ujio wake mpya baada ya kutoka jela.....
No comments:
Post a Comment