Tuesday, August 30, 2011
BEYONCE:NATEGEMEA KUPATA MTOTO JAMANI!!
"Natamani na nyie mpate hisia juu ya penzi hili linaloongezeka ndani ya nafsi yangu''. Beyonce aliyasema maneno hayo kisha kufunua koti alilovaa na kugusa tumbo lake,kisha akautangazia umma wa watu uliokuwa ukimtazama 'live' kwamba kwa sasa ni mjamzito na anatarajia kupata mtoto.
Beyonce Knowlese mke wa mmoja wa wakali wa HipHop Jay-z alizaliwa mnamo mwaka 1980 na katika miaka ya 90 mwishoni na 2000 alikuwa ni mmoja wa wasanii waliokuwa wanaunda kundi la muziki wa R&B la Destiny's Child akiwa na Kelly Rowland pamoja na Michelle Williams. Mwaka 2008 alifunga ndoa na Shawn Cutter ambaye ni msanii mwenye heshima katika muziki wa Hiphop na mjasiriamali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment