Thursday, June 16, 2011

MWANA MAMA AUZA BARUA ALIYOANDIKIWA NA OBAMA ILIKUSAIDIA FAMILIA YAKE.


Destiny Mathis mama wa watoto watatu na umri wa miaka 26,ameamua kuiuza barua aliyowahi kuandikiwa na Rais Obama kwa kiasi cha dola za marekani 11000/- ili kuisaidia familia yake ambayo inatawaliwa na tatizo la kiuchumi. Mwana mama huyo alimwandikia Obama barua mnamo mwezi Novemba mwaka jana akilalamika hali ngumu ya kiuchumi iliyomkumba baada ya kuachishwa kazi kutokana na matatizo aliyopata wakati wa ujauzito wake. Lakini pasi na kutegemea Rais Obama alijibu barua hiyo kwa kumpa matumaini kuwa ataondokana na hali hiyo.
Lakini kutokana na hali ngumu ya maisha inayomkabili mama huyo ameamua kuiuza barua hiyo,ili kuikwamua familia yake na hali ngumu ya maisha.
HII HAPA CHINI NI BARUA ALIYOJIBIWA NA RAIS OBAMA...

No comments:

Post a Comment