Thursday, June 9, 2011
BAJETI YA TANZANIA 2011/2012
Jana Waziri wa Fedha na Uchumi wa Tz Mustapha Mkulo amesoma
bajeti ya Tz. Watu mbalimbali wameizungumzia hiyo bajeti akiwemo Zitto Kabwe ambaye ni Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni ambaye amesema kwa kiasi kikubwa serikali imefuata maoni ya kambi ya upinzani. Kwa mfano Serikali imesema itapunguza kodi ya mafuta,ingawa Waziri hajasema ni kwa kiwango gani watapunguza kodi hiyo. Amesema kambi ya upinzani ilipendekeza kodi ya mafuta ipungue kwa asilimia 40.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof. Ibrahim H. Lipumba amesema bado bajeti ina matatizo kwa sababu inaonyesha matumizi ya serikali ni makubwa kuliko mapato inayotegemea kukusanya. Serikali inategemea kukusanya Trilioni 6 huku matumizi yakiwa ni Trilioni 8.
Unaweza kuisoma bajeti hiyo kupitia tovuti ya wizara ya Fedha ambayo ni http:/www.mof.go.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment