Monday, August 27, 2012



         MCHUNGAJI MTOTO EZEKIEL STODDARD ANA MIAKA 11 NA ANAONGOZA KANISA



Ana miaka 11 tu lakini ameshaanza kuwashangaza watu wengi kutokana na jinsi anavyohubiri neno la Mungu. Ezekiel Stoddard mtoto anayedai kuwa alipata wito wa kumtumikia Mungu miaka miwili iliyopita. Na ilipofika may mwaka huu akawekwa wakfu kuwa mtumishi wa Mungu katika kanisa la Fulliness of Time huko Maryland  Marekani. Wazazi wake wote ni wachungaji wa kanisa hilo. Mtoto Ezekiel anasema ingawa watoto wenzake wamekuwa wakimdhiaki kwamba yeye ni fake pastor lakini uwa hajali hayo yote,bali anasonga mbele.
Ezekiel anasema Mungu alimtokea kwenye ndoto na kumwambia asome Zaburi ya 23. Na alipewa Zaburi
hiyo ili iwe kama muongozo wake. Anasema yeye ni mpenzi wa basketball na tennis na pia anapenda kutazama sinema.






No comments:

Post a Comment