Sunday, October 16, 2011

ACE HOOD:MCHIZI AMBAYE ALIKAMATA PESA YA KUTOSHA KUPITIA MUZIKI LAKINI MWISHO WA SIKU ALIJIKUTA AKIFULIA.


Ace Hood anapatikana kwenye lebo ya muziki inayomilikiwa na Dj Khaled inayokwenda kwa jina la WE THE BEST MUSIC GROUP.
Jamaa amekiri kuwa baada ya kutoa albamu mbili ambazo zilimpa pesa kiaina na kujikuta akiwa na uwezo kununua vitu kadhaa vya thamani ikiwemo mikufu na magari,hatimae alijikuta akifilisika,kiasi cha kushindwa kulipia hata pago la nyumba.
albamu zake mbili za mwanzo ni 'Gutta' pamoja na 'Ruthless' pia akafanya show kadhaa,lakini alijikuta akihishiwa kiasi cha kupelekwa mahakamani na Land lord wake. Ace hood anasema mwisho wa siku ilibidi arudi kwa mama yake na akawa mtu wa kujifungia ndani na akawa mtu anayekwenda kanisani mara kwa mara.
Lakini anasema anamuheshimu na kumshukuru Dj Khaled kwa sababu hakumuacha kwani alikuwa naye bega kwa bega.
Kwa sasa Ace hood ametoa albamu nyingine inayoitwa ''Blood,Sweat and Tears''ambayo inaonekana kufanya vizuri zaidi ya albamu zake zilizopita na pia kwa sasa anatengeneza pesa ya kutosha.
WADAU BILA SHAKA HII ISHU INA MUHUSU KILA MTU,NA NAWEZA NIKASEMA TU KATIKA MAISHA HAUPASWI KUWA MTU WA KUKATA TAMAA.

    

''HUSTLER WILL NEVER GIVE UP,AND HE WILL CONTINUE TO HUSTLE  UNTIL DEATH''

No comments:

Post a Comment