Sunday, July 24, 2011

BIN HAMMAM AFUNGIWA MAISHA NA FIFA


Aliyekuwa mgombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu la dunia FIFA Mohamed Bin Hammam amefungiwa na shirikisho hilo kutojishughulisha na shughuli zozote za uongozi katika mpira wa miguu baada ya kukutwa na hatia katika sakata la kujaribu kutoa rushwa hili achaguliwe kuwa Rais wa shirikisho hilo katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita. Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatari na kiongozi wa zamani wa shirikisho la soka la Asia atotakiwa kujishughulisha na mpira wa miguu katika maisha yake yote.
                                  Hapa Bin Hammam (kulia) akiwa Sepp Blatter Rais wa FIFA.

No comments:

Post a Comment