Monday, October 17, 2011

KWA NINI NIGERIA WAFANIKIWE NA SIO EAST AFRICA?



Unapomuuliza mtu yeyote hapa East Africa kama anaifahamu Nigeria,pasi na shaka yeyote atakujiubu ndio.
Na unapomuuliza anaifahamu vipi Nigeria?,atakujibu anafahamu movies zao,muziki wao,na hata upande wa mpira wa miguu anafahamu. Hii ni kwa nini?
Nigeria kwa muda sasa wanaonekana kukamata akili nyingi za wana-East Africa kwa sababu ya movies zao na hata muziki wao. Kwa upande wa mpira wa miguu wanaonekana kushuka kwa sasa,ukilinganisha zamani.
Ukiwataja wasanii wa muziki kama 2face,D'banj na P'square hayo ndio majina yanayooneka kushika masikio ya wana-East Africa. Ingawa kwa sasa kuna msanii mwingine anaitwa Mr. Flava naye anaonekana kuchukua nafasi.
KWA NINI TANZANIA,KENYA,UGANDA,BURUNDI NA RWANDA HATU SHINE KAMA NIGERIA?
Je kuna tatizo lolote katika aina ya muziki wetu au movies zetu?Ingawa Kenya wanaonekana kung'ara katika mchezo wa riadha. Lakini mchezo wa riadha sio aina ya mchezo unaopendwa sana kama mpira wa miguu.
Kwa sasa hivi muziki wetu unaonekana kuishia hapa hapa tu. Hata soko la movies zetu linaishia hapa hapa tu.
Je tatizo ni lugha,kuwa tunatumia sana kiswahili na wenzetu wanatumia kingereza?
 Nilipata nafasi ya kuongea na mkenya mmoja ambaye kwa mawazo yake,aliniambia Tanzania movie industry yake ni nzuri sana lakini tatizo ni lugha,kuwa kiswahili kinatumika sana. Na alisema ili movie za Tanzania zipate soko nje ya Tanzania inapaswa English ichukue nafasi.
Bongo Fleva,Genge,Kapuka,vipi mbona hatuvuki boda?
Yuko wapi Lady Jaydee,Nonini,Kidumu,Juacali,Chegge,Joh Makini?

Kwa nini Hasheem Thabeet pekee ndiye alifanikiwa kwenda level; ya NBA?
Tumeshuhudia Nigeria ikifanikiwa kwa upande wa movie na inasemekana baada ya Hollywood na Bollywood inayofuatia ni Nollywood. Hata katika soko la muziki Nigeria wapo juu na ilishuhudiwa mwaka huu D'banj na 2face wakichukua tuzo za BET MUSIC AWARDS katika category ya international artists.
Kwa upande wa football wapo kina Mikel Obi wa Chelsea na wengine kadhaa. Ingawa yupo Mariga kutoka Kenya wa Inter Millan.

                                                  I WISH EAST AFRICA TO MOVE ON!!

No comments:

Post a Comment