Thursday, September 8, 2011

RIHANNA AND JAY-Z ''HAKUNA BEEF''


Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa uhusiano kati ya Jay-z na Rihanna hauko sawa,na imedaiwa ni baada ya msanii Beyonce kutangaza kuwa na ujauzito. Ikumbukwe kuwa ni hivi karibuni mwanadada Beyonce aliutangazia umati wa watu uliokuwepo katika tuzo za MTV Music Awards kuwa ana ujauzito. Imeelezwa tukio hilo lilimkera Rihanna na kufikia hatua ya kutaka kuachana na lebo inayosimamia kazi zake ya Roc Nation ambayo inamilikiwa na mume wa Beyonce Jay-z. Na hatimaye imekanushwa na uongozi wa Def Jam ambayo ni kampuni mama inayosimamia kazi za Rihanna.
Ilielezwa kuwa Rihanna alifikia uamuzi wa kuitema RocNation kutokana na kushindwa kuelewana na Jay-z pamoja uongozi mzima wa lebo hiyo katika masuala ya kifedha.

Na muda mchache uliopita katika mtandao wa twitter,Rihanna ameandika yeye ataendelea kuwepo Roc Nation mpaka kifo chake. ''ROCNATION til I die''

No comments:

Post a Comment