Tuesday, August 23, 2011
JAY-Z NA KANYE WEST WAAMUA KUSAIDIA TATIZO LA NJAA AFRICA MASHARIKI
Wasanii kutoka USA Jay-z na Kanye West wanatarajia kuipiga mnada gari aina ya Maybach waliyoitumia katika video yao mpya ya ''Otis". Na wanatarajia pesa itakayopatikana kusaidia tatizo la njaa lililozikumba nchi kadhaa za Afrika Mashariki ambazo ni Somalia,Sudan kusini,Djibouti,Ethiopia na Kenya.
Kwa kawaida gari aina ya Maybach ambayo ni miongoni mwa magari yenye thamani kubwa duniani,inatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola za marekani 300000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 480.
Katika video ya ''otis'' Jay-z na Kanye wanaonekana wakiwa katika gari hilo,ambalo linaonekana kuharibiwa.
Na haijulikani kwanini waliamua kuharibu gari hiyo na baadae kuamua mabaki yake yapigwe mnada kusaidia watu wa Afrika Mashariki. Labda wanataka kutoa ujumbe kwa jamii kuwa "MONEY AINT A PROBLEM" OR ''MONEY DOESNOT COST A THING''.
TAZAMA VIDEO YA ''OTIS'' HAPO CHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment